Waamuzi 8

Alikuwa na wana sabini wa kwake mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na wake wengi.

Judges 8:30 (UKJV) And Gideon had threescore and ten sons of his body begotten: for he had many wives.

28Hivyo Midiani ikashindwa mbele ya Israeli nayo haikuinua kichwa chake tena. Wakati wa siku za uhai wa Gideoni, nchi ikafurahia amani miaka arobaini.

29Yerub-Baali mwana wa Yoashi akarudi kwenda kuishi katika nyumba yake.

30Alikuwa na wana sabini wa kwake mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na wake wengi.

31Suria wake, aliyekuwa anaishi huko Shekemu, pia alimzalia mwana, ambaye alimwita Abimeleki.

32Gideoni mwana wa Yoashi akafa akiwa na umri mzuri wa uzee, na akazikwa katika kaburi la Yoashi baba yake huko Ofra ya Waabiezeri.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.