20“ ‘Wadudu wote warukao ambao hutembea kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu.
21Lakini wako viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi.
22Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi.
23Lakini viumbe wengine wote wenye mabawa na wenye miguu minne ni machukizo kwenu.
24“ ‘Mtajinajisi kwa wanyama hawa. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.