6“ ‘Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Bwana.
7“ ‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye.
8“ ‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako.
9“ ‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.
10“ ‘Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako; utajivunjia heshima.