21Hakuna mzao wa kuhani Aroni mwenye kilema chochote atakayekaribia kutoa sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. Kama ana kilema, kamwe asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake.
22Anaweza kula chakula kitakatifu sana cha Mungu wake, pia hata chakula kitakatifu.
23Lakini kwa sababu ya kilema chake, kamwe asikaribie karibu na pazia wala kukaribia madhabahu, asije akanajisi mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Bwana, niwafanyaye watakatifu.’ ”
24Basi Mose akamwambia Aroni jambo hili na wanawe, pamoja na Waisraeli wote.