26Wale waliosikia haya wakauliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”
27Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.”
28Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwa navyo tukakufuata!”
29Yesu akajibu, “Amin, nawaambia, hakuna hata mtu aliyeacha nyumba yake, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu
30ambaye hatapewa mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya, na hatimaye kupata uzima wa milele ujao.”