40Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza,
41“Unataka nikufanyie nini?” Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”
42Yesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.”
43Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.