28Mambo haya yatakapoanza kutendeka, simameni na mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umekaribia.”
29Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote.
30Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia.
31Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.
32“Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia.