41Sisi tumehukumiwa kwa haki kwa kuwa tunapata tunayostahili kwa ajili ya matendo yetu. Lakini huyu mtu hajafanya kosa lolote.”
42Kisha akasema, “Yesu, unikumbuke utakapokuja katika Ufalme wako.”
43Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”
44Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa,
45kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili.