Luka 23

Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

Luke 23:46 (UKJV) And when Jesus had cried with a loud voice, he said, Father, into your hands I commend my spirit: and having said thus, he gave up the spirit.

44Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa,

45kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili.

46Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

47Yule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.”

48Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.