27“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia.
28Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.
29Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyangʼanya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia.
30Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie.
31Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.