Luka 8

Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.”

Luke 8:20 (UKJV) And it was told him by certain which said, Your mother and your brethren stand without, desiring to see you.

18Kwa hiyo, kuweni waangalifu mnavyosikia. Kwa maana yeyote aliye na kitu atapewa zaidi. Lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho atanyangʼanywa.”

19Wakati mmoja mama yake Yesu na ndugu zake walikuja kumwona, lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu.

20Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.”

21Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulifanya.”

22Siku moja Yesu alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni twende mpaka ngʼambo ya ziwa.” Nao wakaondoka.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.