53Wao wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekwisha kufa.
54Yesu akamshika yule binti mkono na kuita, “Binti, amka!”
55Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara moja. Akaamuru apewe kitu cha kula.
56Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote juu ya yale yaliyotukia.