25Amin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”
26Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.
27Yesu akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “ ‘Nitampiga mchungaji, nao kondoo watatawanyika.’
28Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
29Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”