42Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”
43Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na wazee.
44Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.”
45Mara Yuda akamjia Yesu na kusema, “Rabi.” Akambusu.
46Wale watu wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi.