16Askari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
17Wakamvalisha Yesu joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani.
18Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!”
19Wakampiga kwa fimbo ya mwanzi tena na tena kichwani na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake, wakamsujudia kwa kumdhihaki.
20Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe.