15na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu.
16Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro);
17Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo);
18Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
19na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.