Marko 4

Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema:

Mark 4:2 (UKJV) And he taught them many things by parables, and said unto them in his doctrine,

1Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umekusanyika kumzunguka ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari.

2Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema:

3“Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake.

4Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.