7Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu.
8Wale watu walikula na kutosheka. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba.
9Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga,
10aliingia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda sehemu za Dalmanutha.
11Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.