Marko 9

Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu.

Mark 9:4 (UKJV) And there appeared unto them Elijah with Moses: and they were talking with Jesus.

2Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao.

3Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha.

4Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu.

5Petro akamwambia Yesu, “Rabi, ni vyema sisi tukae hapa. Turuhusu tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.”

6Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.