Mathayo 14

Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

Matthew 14:11 (UKJV) And his head was brought in a charger, and given to the damsel: and she brought it to her mother.

9Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake.

10Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani.

11Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

12Wanafunzi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Yesu.

13Yesu aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.