33Ule umati wa watu uliposikia hayo, ulishangaa sana kwa mafundisho yake.
34Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja.
35Mmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema,
36“Mwalimu, ni amri ipi katika Sheria iliyo kuu kuliko zote?”
37Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’