Mathayo 23

Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu!

Matthew 23:32 (UKJV) Fill all of you up then the measure of your fathers.

30Nanyi mwasema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu, tusingalikuwa tumeshiriki katika kumwaga damu ya manabii!’

31Hivyo mnajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii.

32Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu!

33“Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya jehanamu?

34Kwa sababu hii, tazameni, natuma kwenu manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na kuwafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.