7Hupenda kusalimiwa masokoni na kutaka watu wawaite ‘Rabi.’
8“Lakini ninyi msiitwe ‘Rabi,’ kwa sababu mnaye Bwana mmoja na ninyi nyote ni ndugu.
9Nanyi msimwite mtu yeyote ‘Baba,’ hapa duniani, kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni.
10Wala msiitwe ‘Mwalimu,’ kwa maana mnaye mwalimu mmoja tu, ndiye Kristo.
11Yeye aliye mkuu kuliko ninyi nyote miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.