34Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia.
35Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
36“Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.
37Kama ilivyokuwa wakati wa Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
38Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina.