40Watu wawili watakuwa shambani, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa.
41Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa.
42“Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu.
43Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa.
44Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.