Mathayo 25

Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi.

Matthew 25:17 (UKJV) And likewise he that had received two, he also gained other two.

15Mmoja akampa talanta tano, mwingine talanta mbili, na mwingine talanta moja. Kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri.

16Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi.

17Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi.

18Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alikwenda akachimba shimo ardhini na kuificha ile fedha ya bwana wake.

19“Baada ya muda mrefu, yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.