Mathayo 27

Yosefu akauchukua mwili wa Yesu, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi,

Matthew 27:59 (UKJV) And when Joseph had taken the body, he wrapped it in a clean linen cloth,

57Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yosefu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.

58Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe.

59Yosefu akauchukua mwili wa Yesu, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi,

60na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake.

61Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwepo mahali pale, wakiwa wameketi mkabala na kaburi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.