2Ndipo akaanza kuwafundisha, akisema:
3“Heri walio maskini wa roho, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.
4Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.
5Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi.
6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.