Mathayo 8

Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata.

Matthew 8:1 (UKJV) When he was come down from the mountain, great multitudes followed him.

1Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata.

2Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.”

3Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.