Mathayo 9

Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.”

Matthew 9:29 (UKJV) Then touched he their eyes, saying, According to your faith be it unto you.

27Yesu alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipiga kelele kwa nguvu na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

28Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Yesu akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?” Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.”

29Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.”

30Macho yao yakafunguka. Yesu akawaonya vikali, akisema, “Angalieni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.”

31Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.