23Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase,
24naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini.
25Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.
26Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri,
27naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.