15Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni; kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi; kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;
16kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni; kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;
17kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi; kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.
19Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.