49Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.
50Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Mose,
51“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani,
52wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada.
53Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.