24Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.
25Moyo wa wasiwasi humlemea mtu, bali neno la huruma humfurahisha.
26Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki, bali njia ya waovu huwapotosha.
27Mtu mvivu haoki mawindo yake, bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.
28Katika njia ya haki kuna uzima; katika mapito hayo kuna maisha ya milele.