18Mjinga hurithi upumbavu, bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji.
19Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema, nao waovu kwenye malango ya wenye haki.
20Maskini huepukwa hata na majirani zao, bali matajiri wana marafiki wengi.
21Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji.
22Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu.