5Shahidi mwaminifu hadanganyi, bali shahidi wa uongo humimina uongo.
6Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati, bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.
7Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.
8Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
9Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.