12Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.
13Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza, huo ni upumbavu wake na aibu yake.
14Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?
15Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.
16Zawadi humfungulia njia mtoaji, nayo humleta mbele ya wakuu.