1Mtu ajitengaye na wengine hufuata matakwa yake mwenyewe; hupiga vita kila shauri jema.
2Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe.
3Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia, pamoja na aibu huja lawama.
4Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji, bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.