18Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki, nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu.
19Ni afadhali kuishi jangwani kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.
20Katika nyumba ya mwenye hekima kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta, lakini mtu mpumbavu hutafuna vyote alivyo navyo.
21Yeye afuatiaye haki na upendo hupata uzima, mafanikio na heshima.
22Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu, na kuangusha ngome wanazozitegemea.