28Shahidi wa uongo ataangamia, bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu.
29Mtu mwovu ana uso wa ushupavu, bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake.
30Hakuna hekima, wala akili, wala mpango unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.
31Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Bwana.