8Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini.
9Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo.
10Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.
11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua.
12Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha.