Mithali 31

Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani.

Proverbs 31:22 (UKJV) She makes herself coverings of tapestry; her clothing is silk and purple.

20Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

21Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.

22Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani.

23Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.

24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.