31Pamoja na hayo, kama akikamatwa, lazima alipe mara saba, ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.
32Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.
33Mapigo na aibu ni fungu lake na aibu yake haitafutika kamwe;
34kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume, naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.
35Hatakubali fidia yoyote; atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.