9Watoto wake na waachwe yatima, mke wake na awe mjane.
10Watoto wake na watangetange wakiomba, na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao.
11Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo, matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni.
12Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema wala wa kuwahurumia yatima wake.
13Uzao wake na ukatiliwe mbali, majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.