4Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, lakini mimi ninawaombea.
5Wananilipiza mabaya kwa mema, chuki badala ya urafiki wangu.
6Agiza mtu mwovu ampinge, mshtaki asimame mkono wake wa kuume.
7Anapohukumiwa, apatikane na hatia, nayo maombi yake yamhukumu.
8Siku zake za kuishi na ziwe chache, nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine.