4Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!”
5Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma.
6Bwana huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.
7Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako.
8Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umeniokoa nafsi yangu na mauti, macho yangu kutokana na machozi, miguu yangu kutokana na kujikwaa,