Zaburi 18

Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi.

Psalm 18:12 (UKJV) At the brightness that was before him his thick clouds passed, hail stones and coals of fire.

10Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo.

11Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, hema lake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua ya angani.

12Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi.

13Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

14Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.