1Nakupenda wewe, Ee Bwana, nguvu yangu.
2Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.
3Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
4Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea.