19Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
20Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
21Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
22Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.
23Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.