22Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.
23Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.
24Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.
25Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia.
26Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi.